Salasala, Dar es salaam info@sokohost.co.tz
Follow us:

Huduma Tulizonazo

Tunatoa huduma hizi kwa ubora kabisa ili kutoa matokeo chanya ya kiafya na malengo ya huduma.

Kununua mahitaji

Tunatoa huduma ya kununua bidhaa sokoni kulingana na uhitaji wa mteja, utaweka oda na sisi tutaenda kukununulia sokoni kwa watoa huduma ambao tuliowachagua kwa kukidhi viwango vya ubora na kuipa kipaumbele afya ya mteja, Sokohost hatuna bidhaa za moja kwa moja hivyo unapoagiza ndio tunakufanyia oda yako kwa uharaka na ubora huku tukiilinda na kuiimarisha afya ya mteja.

Soma zaidi

Delivery ( Kufikisha mlangoni)

Tunatoa huduma ya kuleta bidhaa baada ya kununuliwa hadi mlangoni kwako, hii ikimaanisha kuwa ukisha weka oda utaletewa bidhaa hadi mlangoni kwako, kwa kuzingatia hili kwa sasa tunahudumia maeneo ya wilaya ya KINONDONI na UBUNGO na matarajio yetu ni kufikia wateja wote kwa jiji la Dar es salaam na baadae nchi nzima, lakini uharaka na kujali wakati ni jambo la msingi katika utoaji wa huduma yetu hivyo tunazingatia muda na umbali pia.

Soma zaidi

Mpango wa Chakula

Tunatoa huduma ya kutengeneza mpango wa chakula (diet) kwa makundi tofauti tofauti ya uhitaji, ukweli ni kwamba unaweza kuwa unafahamu unatakiwa kula mlo kamili lakini unafahamu mchanganyiko wake ili kukupa kiwango sahihi na ubora kamili kwa afya yako na familia yako?, tunao mpango kwa makundi mbalimbali

Familia, Watu wazima ( wazee), Watoto, Mtu binafsi, Kupunguza uzito, Kuongeza uzito,Wagonjwa ( Kisukari,HIV,Moyo,Vyakula kwa kuongeza aina ya madini ( Calcium,Pottasium,Omega 3-9, n.k)

Soma zaidi

Kuandaa Mboga

Tunatoa huduma ya kuandaa mboga kwa kiwango ambacho utahitaji :- Kukaanga samaki, Kuchemsha nyama, Kuchemsha maharage,Kukata kata mboga mboga n.k, unaweza kuletewa mboga yako ikiwa tayari kabisa ukifika wewe ni kuunga tu na kula chakula chako.

Soma zaidi

Mpishi wa kukodi ( Visiting Chef)

Unashughuli na haujui utapata wapi mpishi mzuri wa kukodi au umechoka na hauwezi kupika vizuri, usijali tunatoa huduma ya kukuletea mpishi wa kukodi ambae atakuja anapika na kuondoka, utachagua mwenyewe jinsi gani akupikie kama hotelini au kama nyumbani kwa gharama nafuu kabisa.

Soma zaidi

Kufundishwa kupika

Tunatoa huduma ya kufundisha kupika kwa pishi unalohitaji kujifunza, tunao wapishi waliobobea na wenye uzoefu wa kutosha kwa mapishi utakayotamani kujifunza ili na wewe uweze kutoa ladha nzuri na afya bora kwa wakati mmoja

Soma zaidi